Burudani

Audio: Rich Mavoko na mama mdogo wa girlfriend wake wazusha ugomvi mzito, amtuhumu kumtafutia wanaume, wafanyiana fujo bar

Rich Mavoko amejikuta akiingia kwenye ugomvi mzito na mwanamke anayeaminika kuwa ni mama yake mdogo na girlfriend wake baada ya kumtuhumu kuwa amekuwa akimtafutia wanaume.

1977416_816482978391474_3724788443506466378_n

Tukio hilo linadaiwa kutokea Jumanne hii huko Tabata Bima jijini Dar es Salaam ambapo mwandishi wa blog ya Tizneez alifanikiwa kurekodi sauti ya tukio zima.

Mavoko alienda kwenye bar moja iliyopo kwenye maeneo hayo ambapo inavyoonekana alimkuta mpenzi wake akila bata na wanaume wengi ambao aliwaanzishia fujo kiasi cha kutengeneza scene! Mwanaume mmoja alijeruhiwa vibaya kwa kupigwa na jiwe.

Katika sauti hiyo, Rich Mavoko anasikika akidai kuwa amepigwa jiwe kwenye jino kufuatia ugomvi huo. “Nimepasuliwa mimi kwasababu ya kuja kumchukua mwanamke wangu,” anasikika Mavoko akiwaambia vijana walioamua ugomvi huo.

“Kwasababu mimi sio chizi nije kumchukua mwanamke wangu kwa vitu vya kipumbavu. Subiri iwake hii simu muone ambayo yameandikwa humu na mama yake mdogo. Mama mdogo anamuambia ‘njoo hapa bar kuna watu wanahitaji company. Mimi sipo nipo kwenye kazi zangu, si mnajua kazi zangu? Niko studio! Narudi nyumbani kwangu sa hizi usiku hamna mwanamke wangu,” anasikika Mavoko kwa sauti yenye taharuki.

“Hata kama nimemkosea, lazima tuongee. Asiweze kuja kukaa bar, anakaaje bar? Lazima tuje sehemu tukae tuongee au sio? Leo nakuja kukuta meseji kwamba njoo hapa bar tuongee.

Je ungekuwa wewe ungefanya nini? mimi nimekuja hapa sijakuja kwa shari, nimemuita mke wangu njoo twende tukagombane nyumbani, lakini nilichokikuta hapa ni tofauti. Mwanamke wangu ananipanikia, ananiambia nitakupiga, nitakuua, mimi nikubali kweli kupasuka?” anasikika akihoji Mavoko.

“Mimi sina mtu niliyempasua hapa, huyu mshkaji kapasuliwa na wao wenyewe, sijashika jiwe mmeniona nimeshika jiwe? Sijashika chupa .
Haifamiki kipi kiliendelea baada ya hapo lakini tumeamua kuzungumza na Rich Mavoko kuhusiana na tukio hilo ambalo awali alituambia kuwa si kweli kwakuwa hayupo jijiniDar es Salaam.

“Tabata sijarudi muda mrefu halafu kama ningekuwa nimegombana ningekuambia ukweli, unaona hata muziki sijatoa muda mrefu, namuuguza shangazi yangu.”

Kuhusu inayosikika ni sauti yake Mavoko anasema, “Sasa kama ni sauti yangu nitakuwa nimegombana lini, labda nimegombana zamani,” alisema. Hata hivyo mwishoni Mavoko amekiri kuwa ni kweli tukio hilo limetokea lakini ni muda mrefu.

“Ni siku nyingi sana, sio jana wala sio juzi, yaani ni ugomvi ambao labda wa kitambo. Hizo zilikuwa issue za mapenzi tu, kwenye mapenzi lazima kuna ugomvi wa hapa na pale.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents