Burudani

AY: Uganda ina industry ngumu sana kuiingia

Ni lini mara ya mwisho umesikia msanii wa Tanzania ameenda kufanya show nchini Uganda? Ukweli ni kwamba, pamoja na kuwa jirani na Uganda, ni ngumu mno kwa msanii wa Tanzania kuingia nchini humo na akafanikiwa. AY anakiri hivyo pia.

AY

“Uganda ni industry ngumu sana kuiingia,”AY ameiambia Bongo5.

“Ndio maana unakuta nikienda show kule Uganda, najikuta mimi ni rapper peke yangu, mimi sijawahi kumuona Navio anaperform kwenye show zangu ambazo nikiitwa kule. Unaweza kujikuta na watu wa ragga, dancehall.”

AY amesema japo si wasanii wengi wa Tanzania wanaenda kufanya show Uganda, wasanii wa Kenya wamekuwa wakienda kwa wingi na anaitaja sababu.

“Ambacho advantage wanaipata Wakenya kwenda sana Uganda sasa hivi ni return ticket. Promota akiangalia kumchukua msanii Tanzania ni dola 500, kumchukua msanii Kenya ni dola 120. Hicho ndio mara nyingi nimewasikia mapromota wakisema, wanaona bora nikwepo gharama.”

Msikilize hapa.

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/118642393″ width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents