Burudani

Baghdad awakutanisha Paka na Chui (Nay wa Mitego na Chidi Benz) kwenye ngoma yake bila wao kujua

Ugumu wa game la muziki nchini umewafanya wasanii wengi kubuni njia mbadala (za kimafia zaidi) kutengeneza ‘keek’ mjini kama wasemavyo vijana wa siku hizi.

Baghadad

Wengine wamewahi kusambaza picha za uongo kuwa walikamatwa na madawa ya kulevya ili kuitengenezea njia nzuri ngoma mpya,(sikumbuki kama stunt hii ilifanikiwa, I guess it flopped). Wengine huyatumia magazeti kutengeneza stunts za kila aina ilimradi tu majina yao yasitoke midomoni mwa mashabiki wa muziki. Njia hii imewasaidia wengi lakini wengine stunts zao ziki’backfire’ na kuwaletea timbwili la kufa mtu mtaani.

So katika muendelezo huo wa kutafuta keek mjini, rapper Baghdad ameamua kuwa ‘kreative’ kidogo. Vipi kama ukiwasikia maadui wawili kimuziki ambao ni kama Paka na Panya kwenye ngoma yake? Inasound poa sio? Rapper huyo ameamua kucheza mchezo ‘mchafu’ kwa kuwakutanisha Nay wa Mitego na Chidi Benz wenye beef bila wao kujua.

Alichofanya Baghdad ni kuwaambia kila rapper katika muda wake kuwa angependa kumshirikisha. Nay wa Mitego alipewa kazi ya kuipamba chorus ya ngoma hiyo iitwayo ‘Waambie Nipo’. Nay bila kinyongo aliingiza sauti zake na mwisho kuweka outro. Kwenye outro Nay anasikika akisema ‘mngenipa hata verse moja tu niwaharibie humu, mna bahati’

Chidi Benz kwa muda wake naye aliingiza verse ya pili kwenye ngoma hiyo bila kujua kuwa adui yake Nay kapita kwenye chorus ya ngoma hiyo. Wasanii hao wawili wamekuja kufahamu mchongo huo jana baada ya kupigiwa simu na Gossip Cop kwenye U Heard ya Clouds ambapo wote waliipokea habari hiyo kwa surprise kubwa.

Nay alichukia kwanini Baghdad hakumwambia kuwa Chidi pia atakuwemo humo na kwamba hata kama angemwambia ukweli asingekataa kufanya kwakuwa yeye ni mfanyabiashara. Hatua hiyo imemfanya Nay akatae tena kuendelea kufanya video ya wimbo huo licha ya kuwa tayari alishashoot baadhi ya vipande.

Hata hivyo Chidi Benz habari hii aliipokea kwa jaziba na kumtaka Baghdad aitoe verse yake kwenye wimbo huo, jambo ambalo halijafanyika kwakuwa tayari wimbo umetoka. Kwa lugha rahisi ni kwamba Baghdad kaharibu kwa rappers wote na huenda wameshampigia simu kumchimba mkwara. Unakionaje kitendo hicho cha Baghdad kuwakutanisha maadui kwenye wimbo wake bila wao kujua?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents