Burudani

Ben Pol kusheherekea birthday yake Jumatatu (Sept 8) na watoto wenye maradhi mbalimbali walioko Muhimbili

Jumatatu ya Tarehe 8 septemba ni siku ya kuzaliwa mwimbaji wa R&B Tanzania, Ben Pol. Na katika kusheherekea siku hiyo mwimbaji huyo wa ‘Jikubali’ ameiambia Bongo5 kuwa atajumuika na watoto wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali walioko katika hospitali ya Muhimbili kitengo cha MOI, ili kuwapatia misaada.

benpol(2)

“Nimefikiria kutembelea kitengo cha watoto hasa watoto wenye matatizo ya uvimbe wa kichwa wale ambao wako MOI, nimeamua mimi pamoja na ndugu na marafiki na watu wote ambao watapenda kujumuika waungane na mimi pia hiyo Jumatatu tarehe 8 mwezi wa tisa saa sita mchana pale MOI. Mimi nitakuwepo nitakuwa napokea marafiki, wageni mashabiki ambao watapenda kujumuika pamoja na wenyeji wetu pale walezi wauguzi pale watatukaribisha, tutajumuika nao tutatoa zawadi ambazo tutakuwa tumejaaliwa siku hiyo then jioni ndo tunaweza kuzungumza mambo kama ni party na nini.” Amesema Ben Pol.

Kupitia Instagram pia amepost:

Ben Pol bday

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents