HabariMichezo

Berlin: Wanawake kuruhusiwa kuogelea bila nguo za juu

Wanawake jijini Berlin nchini Ujeruman hivi karibuni wataruhusiwa kwenda kwenye mabwawa ya kuogelea ya umma bila nguo zinazo ziba sehemu ya juu ya mwili (top) kama ilivyo kwa Wanaume, serikali ya jimbo la Berlin imesema.

Sheria hiyo mpya ya kuogelea inayo ruhusu kila mtu kuogelea bila kufunika mwili wake imekuja baada ya malalamiko ya kubaguliwa kwa mwanamke mmoja ambaye hakuruhusiwa kwenda bila nguo inayoziba sehemu ya juu ya mwili (top) katika bwawa la kuogelea kwenye mji huo.

Mwanamke huyo, ambaye utambulisho wake haukufichuliwa, alizitaka mamlaka kwenye ofisi ya seneti kutenda haki sawa na wanaume kuogelea kifua wazi.

Imeandikwa na @fumo255

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents