HabariSiasa

Bilionea ashinda uchaguzi Lesotho

Tajiri aliyegeuka mwanasiasa ameshinda uchaguzi wa bunge nchini Lesotho, akikosakosa kushinda wingi wa viti wa kutosha kumaliza mkwamo wa kisiasa wa muda mrefu katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Chama cha Revolutionary for Property kilichoundwa miezi sita iliyopita na tajiri huyo milionea, Sam Matekani kimeshinda viti 56 katika bunge la Lesotho lenye jumla ya viti 120, ikiwa ni kwa mujibu wa matokeo ya mwisho yaliyochapishwa na tume ya uchaguzi.

Kwa mwongo mzima nchi hiyo ndogo ya kifalme imekuwa ikiongozwa na serikali za muungano wa vyama, ambazo aghalabu zimekuwa dhaifu na zenye migawanyiko mikubwa.

Hakuna waziri mkuu hata mmoja aliyeweza kukamilisha muhula wa miaka mitano. Matekani amesema ananuia kutumia maarifa ya kibiashara kuupiga jeki uchumi na kushughulikia changamoto za madeni na ukosefu wa ajira.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents