Habari

Bondia Francis Cheka arudi shule ‘Pre-form one’, St Joseph

Bingwa wa dunia wa WBF Francis Cheka ameamua kurejea darasani kujiunga na pre-form one, St Joseph ili kujiendeleza kielimu

Francis Cheka mashine

Cheka amelimbia gazeti la Mwananchi kuwa hakupata nafasi ya kuendelea na shule kutokana na matatizo ya kifamilia na kuishia darasa la saba, ila kwasasa ameamua kurejea darasani baada ya kupewa udhamini na shule ya St Joseph.

“Nahitaji kuwa Cheka mpya kielimu ili nifike mbali, miaka kumi ijayo hadi namaliza elimu yangu nitakuwa na miaka 41. Hapo nitaamua niendelee na ngumi au nifanye biashara zangu nyingine“. Alisema cheka.

Mpiganaji huyo wa masumbwi pia amefunga kiwanda cha kusaga chupa nyumbani kwao Morogoro baada ya kununua mashine ya milioni 8 hali iliyosaidia kuajiri vijana wasio na kazi zaidi ya ishirini na tano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents