Burudani

Cassper Nyovest ajiondoa kuwania nafasi ya kuingia kwenye tuzo za MTV EMA ambazo Diamond ni Nominee!

Rapper wa Afrika Kusini, Cassper Nyovest amesusia tuzo za 2015 MTV Europe Music Awards (MTV EMA) kutokana na kuhisi kuwa hajatendewa haki.

cassper

Jumanne Sept 8, MTV walitangaza majina ya nominees 4 wa kipengele cha ‘Best African Act’ akiwemo Diamond Platnumz, na ikabaki nafasi ya msanii mmoja ambayo waliweka majina ya wasanii watano wapigiwe kura kupata mmoja wa kukamilisha nominees 5 wa kipengele hicho.

Wasanii waliowekwa kupigiwa kura na mashabiki kupitia Twitter kuwania nafasi hiyo moja ni Wizkid (Nigeria), K.O (South Africa) Dj Arafat (Ivory Coast), Stonebwoy (Ghana) pamoja na Cassper Nyovest (South Africa).

Rapper huyo kupitia Instagram yake amesema, kutokana na kwamba hakuchaguliwa kuwa nominee wa kipengele hicho bila kupigiwa kura kama wasanii wenzake wakina Diamond, Davido, Yemi Alade na mpinzani wake mkubwa AKA, basi anaona labda hakustahili nafasi hiyo hivyo haoni haja ya kuomba kura ili achaguliwe kuwa nominee na ndio sababu ameamua kujitoa.

“MTV just announced that I’m one of the people who have to get people to vote for them to be nominated for Best African Act. As I sit here and I think, It may be such an honor&an opportunity but if I’m not nominated with all the other nominees that don’t HAVE 2 vote then maybe I don’t deserve it. In that case, I have decided to stay out of this one. Good luck to all of the nominees. I’d rather spend me time trying to #FillUpTheDome!!! Shout out to all the fans that wanted to vote&those that are already voting but let’s let this one go. Let’s focus on filling up the dome!!!” – Cassper Nyovest

2015 MTV EMAs zitatolewa October 25 jijini Milan, Italy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents