Burudani

Cassper Nyovest aweka historia kwa kuwa msanii wa kwanza wa Afrika Kusini kujaza ukumbi wa watu 20,000

Rapper wa Afrika Kusini, Cassper Nyovest ameweka historia kwa kuwa msanii wa kwanza wa nchi hiyo kujaza ukumbi wa The Dome ulioko jijini Johannesburg kwenye show aliyoandaa mwenyewe iliyofanyika Jumamosi Oct.31.

cassper soldout

Cappser pia ndiye msanii wa kwanza wa Afrika Kusini kuutumia ukumbi huo wenye uwezo wa kujaza watu 20,000 ambao hutumika zaidi kwenye show zinazokuwa na wasanii wa kimataifa.

cassper dome-2

Show hiyo imemgharimu Cassper Rand milioni 4 (zaidi ya shilingi milioni 630) katika maandalizi.

cassper dome

Rapper huyo amejiwekea malengo ya kuweka rekodi nyingine mwakani, kwa kuahidi kufanya show nyingine kwenye uwanja mkubwa zaidi wa ‘Orlando stadium’ wenye uwezo wa kujaza watu 40,000 ambayo ni mara mbili ya The Dome.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents