Burudani

Chris Brown akava jarida la Billboard, azungumzia jela, Rihanna, majuto na maisha mapya

Wakati anajiandaa kutoa album yake ya sita, X, itakayotoka September 16, Chris Brown amekava jarida jipya la Billboard.

chris-brown-billboard

Akiwa na nywele za blonde na kofia nyeusi na tattoo zake zikienea kifuani mwake, kava la jarida hilo lina maandishi yasemayo: Maybe I was out of control.” Katika interview yake hiyo ya kwanza tangu atoke jela, Brown anazungumzia kuhusu album yake ya X, maisha ya jela, Rihanna na kuendelea na maisha mengine.

“Nimegundua kuwa kila nachokifanya kwa kuishi hufungua maisha kwa umma kunichunguza na kwamba nina wajibu kwa kila mmoja kwasababu ya exposure hiyo,” anasema.

“Naweza kusema kwamba mimi ni binadamu tu na nimefanya makosa. Naweza kusema kwamba najaribu kuishi katika njia ya ukweli, uaminifu niwezavyo. Mimi si mkamilifu, hakuna aliye. Hakuna aliye mgumu kwangu kunizidi. Hakuna anayeweza kumfurahisha kila mtu. Hakuna anayeweza kuishi katika maisha yaliyopita na akatarajia kukua. Nimesonga mbele na naamini kuwa sitafsiriwi kwa wasaa mchache tu katika maisha yangu lakini kwa wasaa wote utakaotengeneza maisha yangu.”

Habari nzima ya alichoongea staa huyo itatoka weekend hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents