Burudani

‘Come Over’ ya Vanessa Mdee itaisogolea ‘Closer’?

Ni takriban mwaka mmoja sasa tangu wimbo wa kwanza wa Vanessa Mdee, Closer utoke. Tangu atoe Closer pamoja na video yake, Vanessa aka Vee Money amesikika kwa walau mara mbili kwenye nyimbo alizoshirikishwa ambazo ni Monifere ya Gosby na Bashasha ya Bob Junior.

1425776_706331612719090_1956485625_n

Baada ya kufanya vizuri na Closer ambayo ilisaidia kuwaaminisha watu kuwa ni kweli ni muimbaji mzuri, watu wengi wanausubiria ujio wake mpya ili kuona kama anaweza kuendeleza mfululizo wa hit. Jibu la swali hilo litajulikana leo.

Cha kujiuliza kwenye Come Over ni kama atarap na kuimba pia kama alivyofanya kwenye Monifere na kwenye nyimbo zingine za B’Hits ama ataimba mwanzo mwisho kama kwenye Closer.

Kipya kwenye Come Over ni kuwa awamu hii wimbo wake umefanywa na producer tofauti na aliyemzoea, Pancho Latino. Huu umetengenezwa na member wa kundi la Navy Kenzo, Nahreel.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents