Habari

Dada wa Rais Trump adai kaka yake muongo na asiye na maadili

Dada wa Rais Donald Trump na jaji wa zamani nchini humo amesema kaka yake ni muongo ambaye ”hana maadili”, rekodi ya siri imebaini.

Donald Trump's sister Maryanne Trump Barry secretly recorded ...

Kauli hiyo ya kukosoa iliyotolewa na Maryanne Trump Barry ilirekodiwa na mpwa wake, Mary Trump ambaye mwezi uliopita alichapa kitabu kilichomkosoa rais huyo.

”Tweet yake na uongo, oh Mungu wangu,” Bi Barry alisikika akisema. ”Ni uongo na ukatili.”

Mary Trump amesema alimrekodi shangazi yake kujikinga asiingie matatani.

Trump alijibu katika taarifa yake ailiyotolewa na Ikulu ikisema ”Kila siku kuna jambo jipya, nani anajali.”

Rekodi hizo kwa mara ya kwanza ziliripotiwa na gazeti la The Washington Post ambapo baadae shirika la habari la AP lilizipata.

Trump's sister, a former judge, heard on audio criticizing the ...

‘Alifanyiwa mtihani na mtu’

Katika rekodi hiyo ya siri, Bi Barry amekosoa sera ya uhamiaji ya utawala wa Trump, ambayo imesababisha watoto kushikiliwa kwenye vituo vya wahamiaji kwenye mpaka.

Moja kati ya madai ya Mary Trump kwenye kitabu -Too Much and Never Enough: Enough: How My Family Created the World’s Most Dangerous Man’ ni kwamba mjomba wake alimlipa rafiki yake ili amfanyie mtihani ili aweze kuingia chuo kikuu.

Bi Barry alielezea suala hili kwenye mazungumzo, hata kusema kuwa anakumbuka jina la rafiki aliyehusika kwenye udanganyifu huo.

”Aliingia Chuo Kikuu cha Pennsylvania kwasababu kuna mtu alimfanyia mtihani,” alisema.

Bi. Barry amekuwa akimuunga mkono kaka yake na awali alisema kuwa wawili hao wako karibu. Alishawahi kueleza jinsi Trump alivyokuwa akimtembelea kila siku alipokuwa hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji.

kumlipa Stormy Daniels

Jaji wa Mahakama Kuu katika jimbo la California alimuamuru rais kumlipa Stephanie Clifford, ambaye alifahamika kwa jina la Stormy Daniels kiasi cha dola za kimarekani 44,100.

Kiasi hicho kilitolewa ili kulipa gharama zilizohusu hatua ya makubaliano ya kutotoa taarifa kuhusu mahusiano yao.

Bi. Daniels alidai kuwa yeye na bwana Trump walifanya ngono katika chumba cha hoteli Lake Tahoe, eneo lililo kati ya California na Nevada, mwaka 2006.

Rais Trump amekana kuwahi kuwa na mahusiano hayo

Bi. Daniels amesema alitia saini makubaliano ya kunyamaza kimya kwa gharama ya dola 130,000 mwezi Oktoba mwaka 2016, siku kadhaa kabla ya uchaguzi wa urais.

Katika uamuzi wa mahakama uliochapishwa mtandaoni, jaji aliamua kuwa pamoja na kesi kufutwa, Bi. Daniels alikuwa mshindi katika kesi hiyo, hivyo gharama zake zilipaswa kulipwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents