Burudani

Damian Soul aingia studio kufanya collabo na Nameless wa Kenya

Ambwene Yessaya ‘AY’ ambaye alikuwa ‘mentor’ wa Damian Soul kwenye shindano la Maisha Superstar lililofanyika mwaka huu, aliwahi kusema kuwa wasanii wengi wakubwa wa Afrika Mashariki wamekuwa wakiomba kufanya collabo na Damian, baada ya kuona uwezo wake mkubwa aliouonesha kwenye shindano hilo.

AY-NA-DAMIAN

Damian Soul ambaye ameenda Kenya kufanya media tour, pia ameingia studio kurekodi collabo na msanii mkubwa wa huko, Nameless.

damian Kenya

Kupitia Instagram Damian ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa Reggae ‘Tudumishe’, amepost picha akiwa kwenye studio ya producer Mtanzania Sappy iliyoko Nairobi, pamoja na Nameless na kuandika kuwa wanapika collabo.

“Studiotime Na my Broda @namelesskenya the legend Himself… Bonge moja la vibe yaan Bonge moja la Ngomaaaaa sambamba na producer Hataree @dr_sappy aliefanya XO ya @joh_makini #AmaizingSong #StayTune #goodtimes #Goodmusic4All #GoodmusicNeverDie #MediatourNairobiKenya”

Miongoni mwa wanamuziki walioonesha nia ya kutaka kufanya kazi na Damian baada ya shindano la Maisha Superstar ni pamoja na Jose Chameleone na Erick Wainaina.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents