Bongo5 Exclusives

David Blaine akaa siku tatu katikati ya umeme wa volts milioni moja

‘Mjasiriahatari’ (Daredevil) wa Marekani David Blaine amefanikiwa kumaliza mtihani (stunt) hatari zaidi aliyowahi kuifanya na kuhusisha umeme.

Mwana ‘mazingaombwe’ huyo alikaa siku tatu akiwa amesimama katikati ya mkondo wa umeme wenye volts milioni moja huko jijini New York.

Msemaji wa Blaine alisema jamaa huyo aliweza kutembea kwa kusaidiwa, kuongea na kumbusu mpenzi wake Alizee Guinochet (ah-LEE’-zay gwee-noh-SHAY’) kabla ya kupelekwa hospitali kufanyiwa uchunguzi.

Stunt hiyo ilipewa jina la “Electrified: One Million Volts Always On.” Ambayo ilioneshwa moja kwa moja YouTube kwa msaada wa Intel Corp.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents