Burudani

Davido asema ana mpango wa kufanya collabo na Drake

Hit maker wa ‘Aye’ na mshindi wa tuzo ya BET 2014 ‘Best International Act Africa’, David ‘Davido’ Adeleke wa Nigeria amesema yuko kwenye mipango ya kufanya collabo ya kimataifa na rapper Drake.

davike

Kwa mujibu wa Nigeria Film, Davido amesema tayari ameanza mazungumzo na star huyo kuhusu collabo hiyo anayotarajia itakuwa kubwa.

“Nina mipango ya kufanya collabo na Drake. Ninapenda aina ya muziki wake. Itakuwa ni bomu! Kitu ambacho mashabiki wangu watafurahia. Tayari tuko kwenye mazungumzo juu ya hilo.
Alisema Davido.”

Wakati Davido yuko kwenye mpango wa collabo na Drake, mpinzani wake mkubwa kwa Nigeria, Wizkid tayari amethibitisha kuwa amefanya collabo na aliyekuwa adui wa Drake, Chris Brown ambao kwa sasa wamemaliza tofauti zao na kuwa washkaji tena.

Kibongo bongo tungeweza kupata taswira kama hiyo kama Alikiba akipata collabo na Wizkid, baada ya Diamond kuwa ameshafanya collabo na Davido!

Source: Nigeria Film

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents