Burudani

Dayna Nyange atoa sababu ya kushindwa kufanya collabo na wasanii wa nje

Dayna Nyange amefunguka sababu ya kushindwa kufanya collabo muda wote na wasanii ambao ni rafiki zake kutoka nje.

Dayna

Miezi kadhaa iliyopita muimbaji huyo alidai kuwa ana urafiki wa karibu na baadhi ya wasanii kutoka nchini Uganda akiwemo Cindy, Alicios na wengine wengi.

Akiongea na Bongo5, Dayna amesema kuwa amekuwa na mipango hiyo ya kufanya nao collabo wasanii hao ambao ni watu wake wa karibu ila mpaka pale mipango yake itakapokuwa sawa.

“Mipango ninayo ila sina haraka sana na hilo kwa kuwa nikiwa na utayari kila kitu kitakuwa sawa niko na malengo kadhaa yakitimia ndio nitapiga hatua nyingine,” amesema Dayna.

Kwa sasa msanii huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Komela’ ambao amemshirikisha Bill Nas.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents