Diamond atajwa kuwania tuzo za MTV Europe, #MTVEMA

Majina ya wasanii wa Afrika watakaowania tuzo za MTV Europe, MTVEMA yametangazwa na Diamond ni miongoni mwa wasanii watakaowania tuzo hizo zitakazotolewa November 9 jijini Glasgow, Scotland.

Diamond-600-x-450

Diamond atachuana na Davido, Toofan wa Togo na Goldfish wa Afrika Kusini.

Davido-600-x-450
Kwa mara nyingine tena Davido anachuana na Diamond kwenye tuzo kubwa baada ya ile BET Awards

Hata hivyo mashabiki mwaka huu wamepewa fursa ya kumtaja msanii mwingine wa tano atakayewania tuzo hiyo. Wasanii sita wanaowania nafasi iliyosalia ni:

Anselmo Ralph – #NominateAnselmoRalph
Gangs of Ballet – #NominateGangsOfBallet
Mafikizolo – #NominateMafikizolo
Sarkodie – #NominateSarkodie
Sauti Sol – #NominateSautiSol
Tiwa Savage – #NominateTiwaSavage

Kura za wild card kupitia Twitter zitafanyika hadi September 14 na majina yote ya “2014 MTV EMA” yatatangazwa September 16 na upigaji kura kuanza rasmi.

Soma zaidi kuhusu tuzo hizo hapa

Katika hatua nyingine msanii huyo ameshinda tuzo ziitwazo Afro Australia Music & Movie Awards AAMMA2014 kwa wimbo alioshirikishwa na Dezert Eagle ‘Everyday kama wimbo bora wa kushirikiana.

Related Articles

Back to top button