Burudani

Diamond: Nilivyofika Nigeria nilikuwa najiona kama mkiwa, siwaoni wasanii wenzangu hata Ally simuoni

Baada ya Diamond Platnumz kutua jijini Dar es salaam December 2 akitokea Afrika Kusini akiwa na tuzo zake 3 za Channel O, alikutana na wadau, mashabiki pamoja na waandishi pale Escape 1 kuzungumzia ushindi wake na safari nzima ilivyokuwa.

diamond2

Miongoni mwa maeneo aliyozungumzia ni pamoja na umoja unaohitajika kwa wasanii wa Tanzania ili waweze kuwa wengi katika majukwaa ya kimataifa.

“Ombi langu mimi kiukweli ni moja tu, Unajua lazima kama alivyosema mheshimiwa hapa muziki wetu ushakuwa, watu wanaukubali na tushaona njia kama tunaweza so lazima sisi tujiamini wenyewe tusikaekae sana nyuma kwasababu watu kuna ile kuogopa cha kuona kama aah watanipokea kweli. Na zile za aah ntashindwa kuongea kizungu ntachekwa mi nishachekwa sana kwenye kizungu sana, lakini saizi naweza nikaingia hata Big Brother na broken zangu hivyo hivyo lakini napita hivyo hivyo nimeingia pale juzi Fally hajaongea mi nimeongea “.

Diamond pia ameendelea kuwaomba wasanii wenzake kutotengenezeana beef za wenyewe kwa wenyewe, na hakusita kumtaja Ally Kiba wakati akitoa mifano alipokuwa Nigeria na kujiona yuko peke yake hakuna msanii yeyote wa nyumbani zaidi yake.

“Kingine mimi nilikuwa nataka niombe tufute zile zama zakutengenezeana matatizo wasanii wenyewe kwa wenyewe wa Tanzania kwasababu haiwezi kutusaidia kabisa, alikuwa anaongea kitu mkubwa hapa, nilivyofika Nigeria nilikuwa najiona kama mkiwa kwasababu niko peke yangu, nikiangalia huku simuoni hata Jaguar, huku siwaoni wasanii wenzangu namtafuta Dimpoz namtafuta nani, hata Ally simuoni yaani niko peke yangu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents