Burudani

Diddy na Drake wadaiwa kumaliza beef yao

Inasemekana kuwa marapper Diddy na Drake ambao waliingia kwenye beef mwishoni mwa mwaka jana, wamemaliza tofauti zao.

diddy and drake2

Mastaa hao waliingia kwenye beef baada ya Diddy kumpa konde Dreezy nje ya Club Liv huko Miami December 2014 mwaka jana, kwa madai kuwa Drake alimkosea heshima. Ugomvi wao uliibuka baada ya producer Boi-1da kuwagonganisha kwa kuwapa beat moja.

Kwa mujibu wa TMZ, vyanzo vya karibu vimesema kuwa mastaa hao wamepatana katikati ya mwezi uliopita (April) baada ya kupigiana simu na kuamua kusahau yaliyopita.

Miongoni mwa sababu kubwa zilizotajwa za wao kuamua kupatana, ni kuwa Drake na Diddy wana ratiba za kuhudhuria matukio mengi ya kiburudani kama matamasha, hivyo wakaona haitaleta picha nzuri kama watakuwa wakikutana kwenye matukio hayo huku wakiwa bado hawana maelewano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents