Burudani

DJ mdogo zaidi wa Afrika Kusini mwenye miaka 3 ashinda shindano la SA’s Got Talent 2015 (video)

DJ Arch Jnr ndiye DJ mdogo zaidi wa Afrika Kusini aliyeibuka mshindi wa shindano la South Africa’s Got Talent 2015 na kuondoka na zawadi kubwa ya R500,000 (shilingi milioni 75) baada ya kuwashinda washiriki wengine sita katika fainali iliyofanyika Jumapili ya Nov.8 jijini Johannesburg.

dj Arch

Oratilwe Hlongwane a.k.a DJ Arch Jnr mwenye umri wa miaka 3 ndiye mshindi wa kwanza mwenye umri mdogo katika historia ya mashindano hayo.

Baba yake mzazi Glen Hlongwane amesema kuwa mtoto wake DJ Arch Jnr ameanza ku-Dj akiwa na mwaka 1 ndipo walipogundua kipaji chake.

DJ Arch Jnr alianza kufahamika kwenye mitandao baada ya familia yake kuwa inaweka video zake Youtube akifanya u-dj. Kwenye moja ya video hizo alionekana akiwasha mwenyewe mashine za Udj, na kuweka cds na kuanza kufanya yake.

https://youtu.be/f1ooAG-IOpQ

Mtazame hapa baba yake akihojiwa kuhusu kipaji cha mwanaye baada ya kutangazwa mshindi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents