Habari

Dr Adelhem Meru awashauri waajiri kuielewa vizuri zana ya usalama na afya mahali pa kazi

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) Dr Adelhem Meru, amewashauri waajiri nchini, kuielewa vizuri zana ya usalama na afya mahali pa kazi, na hivyo kuhakikisha wanalinda afya na usalama wa wafanyakazi wao, ili waweze kuzalisha kwa wingi na kufikia malengo waliojiwekea.

Kauli hiyo imetolewa mjini Morogoro wakati wa kikao kazi baina ya Wakala wa Usalama na Afya Mahalipa Kazi (OSHA) pamoja na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA) mkoani Morogoro kwenye kikao kazi ambacho pia kilikuwa na lengo la kuitambulisha kampeni ya vision zero mkoani Morogoro kampeni maalumu ambayo inalenga kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi.

Dr.Meru amesema endapo waajiri hawatazingatia masuala ya usalama na afya, hawataweza kufikia malengo yao waliojiwekea ambao ni lengo kubwa la mfanyabiashara. Amesema hayo hayatawezekana endapo wafanyakazi hawatawekewa mazingira bora ya afya zao na usalama wao.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi, Bi. Khadija Mwenda amesema waliona kuna umuhimu OSHA kushirikiana na TCCIA katika kuhakikisha wanashughulikia kero na changamoto za wafanyabiashara nchini, kwani mchango wao ni mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

Bi. Khadija MwendaAmesema OSHA imetekeleza Andiko la Blue print kwa kiasi kikubwa kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyabiashara nchini, kwa kuondoa tozo mbalimbali ambazo zilikuwa kikwazo kwa wawekezaji na wafanyabishara nchini.

Naye Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Morogoro ndugu Mwadhini Omari Myanza amesema ameishukuru OSHA kwa kutekeleza ipasavyo yale yote yalioelekezwa kwenye Blue Brint, na hivyo kuwasaidia wadau wao.

Kwa upande wake, washiriki wamesema Kikao hicho kimewasaidia na kuwajengea uelewa mpana zaidi masuala ambayo walikuwa hawayaelewi na hivyo yatawasaidia katika shughuli zao wanazozifanya kwa kuhakikisha mazingira ya wafanyakazi yanaboreshwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents