Bongo Movie

Dr Cheni afunguka baada ya kuzushiwa kifo

Baada ya kuzushiwa kifo, msanii wa filamu, Dr Cheni amesema kuwa sio jambo la burasa kuzishiana kifo.

Dr Cheni akiwa na JB
Dr Cheni akiwa na JB

“Jaman kifo kipo na hakuna atakaye kwepa ni lazima tutakufa na hakuna atakayebakia ila si vyema kunizushia, siku yangu itafika tu na wote mtajuwa lakin si jambo la busara kunizushia,” ameandika kwenye Instagram.

Naye Lulu aliandika: Jamaani kuna mambo ya kuzushiana lakini sio KIFO,kuna habari zimezushwa kwamba @drchenitz Cheni amefariki….ni habari za uongo jamani….yuko salama kabisa na juzi ameruhusiwa kutoka hospital na anaendelea vzr…Tunajua kufa ni wajibu lkn mpk Mungu mwenyewe apende…!!!!Pole baba angu.”

Dr Cheni alilazwa May 6,mwaka huu katika hospitali ya Buruhani na kuruhusiwa May 9 baada ya kuugua ugojwa wa Dengue uliosababisha aishiwe nguvu na kupungukiwa damu mwilini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents