Michezo

FA lazitupa t-shirt 4,000 zenye nukuu ya Sam Allardyce zilizokuwa zigawiwe baada ya mechi ya England na Malta

Chama cha soka nchini Uingereza, FA kimelazimika kuzitupa t-shirt 4,000 zilizokuwa zimepangwa kugawiwa kwa mashabiki baada ya mechi ya England na Malta sababu zilikuwa na nukuu ya kocha aliyetimuliwa, Sam Allardyce.

38e1805900000578-3814015-image-a-2_1475169064423

Allardyce, 61, alikuwa akijiandaa na mechi na mechi October 8 lakini kibarua chake kiliota mbawa baada ya kashfa yake ya rushwa kuibuliwa.

FA ilitaka kuzitumia t-shirt hizo kama kumbukumbu ya mchezo wake wa kusaka nafasi ya kushiriki kombe la dunia. Zilikuwa zimeandikwa ‘The journey starts with us all pulling together’ — kitu ambacho Allardyce alikisema siku ameteuliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents