Technology

Fahamu tofauti ya TECNO CAMON 20 na CAMON 20 toleo la Dooble

TECNO kwa Mwaka huu wa 2023 imeachia Toleo la CAMON 20 ya Magic Skin na CAMON 20 Toleo la Bwana Dooble. Hamna tofauti kubwa ya features za ndani kati ya simu hizi isipokuwa TECNO CAMON 20 Toleo la Bwana Dooble ni 5G zote yani CAMON 20 Pro ya Doodle ni 5G na CAMON 20 Premier ya Doodle ni 5G. Utofauti wa simu hizi unapatikana katika muundo wa Sanaa CAMON 20 Toleo la Doodle ina mtindo wa michoro ya Doodle katika jalada la nje na CAMON 20 toleo la awali ina mtindo wa Magic Skin. https://fb.watch/mRA7AgVNmV/?mibextid=cr9u03 

TECNO CAMON 20 toleo la Doodle wakati wa usiku.

Toleo la awali ambalo ni magic skini muundo wake wa Sanaa ya mtindo umetengenezwa kwa ubunifu wa material hairuhusu kukwaruzika lakini pia endapo ikichafuka ni rahisi kusafishika na kurudi katika muonekano wa upya ila kwa Bwana Dooble ujuzi umeongezwa zaidi.

Camon 20 Series ya Mr Dooble hutumia teknolojia ya kubadilisha rangi kulingana na mabadiliko ya tabia ya Mwezi, inachanganya michoro ya graffiti ya Mr Dooble na muundo wa kipekee wa 3D wa CAMON 20. Jalada la nyuma hufyonza mwanga wakati wa mchana na kuiachilia kama umeme wakati wa usiku, na hivyo kuruhusu sehemu ya nyuma ya simu kuonyesha kazi za graffiti za Mr Dooble. Muundo wa kipekee wa Toleo la Mfululizo la CAMON la CAMON 20 la Mr Dooble huifanya kuwa aikoni ya mitindo wakati wa mchana na kuvutia macho wakati wa usiku, na kuifanya kuwa bora kabisa inayochanganya mitindo na Sanaa.

TECNO CAMON 20 Toleo la awali

TECNO CAMON 20 Toleo la Dooble ina mandhari iliyogeuzwa kukufaa kwa mtindo wa grafiti ya Bw. Dooble, AR SHOT na AOD, hivyo basi huwaletea watumiaji mshangao zaidi ya kuonekana.

Simu hizi mahiri TECNO CAMON 20 pro na TECNO CAMON 20 Premier zinaashiria maana halisi ya ubunifu na mabadiliko ya teknolojia simu hizi haziwasilishi mvuto wa nje tu bali pia iko vyema katika kupiga picha na kurecord video za simu.

TECNO CAMON 20 Pro 5G Dooble ina camera kuu ya Megapixel 64 nyuma (Night Potrait Master), 32MP Selfie Camera, 33W flash charge 5000mAh, 256GB ROM + 8GB RAM. 

TECNO CAMON 20 Toleo la Dooble wakati wa mchana

CAMON 20 Premiere 5G Doodle ina camera kuu ya Megapixel 108 wide angle (Night Portrait Master), 32MP Selfie Camera, 45W flash charge 5000mAh, 512GB ROM + 8GB RAM.

Simu hizi zinapatika katika maduka yote ya simu lakini pia @tecnomobiletanzania wameweka huduma ya mkopo bila ya Riba kwa wataopendezwa kumiliki simu hii ya kisasa na kushuhudia ubunifu mpya wa simu hii inavyog’aa wakati wa giza.

Tembelea @tecnomobiletanzania au piga namba 0714029870 kwa huduma ya haraka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents