HabariSiasa

Gerson Msigwa: Taarifa ya ajali ya ndege bado haijatoka

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amesema kwamba serikali bado haijatoa taarifa ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Presicion Air iliyotokea Novemba 6, 2022, hivyo taarifa inayosambaa mitandaoni ipuuzwe kwani haijatolewa na mamlaka rasmi za serikali.

Taarifa hiyo ameitoa hii leoe Novemba 23, 2022, kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema kwamba taarifa kamili itakapokuwa tayari wananchi watajulishwa.

Mbali na hilo ameongea kupitia TBC Taifa na kutolea ufafanuzi juu ya habari hizo za uongo zilizosambazwa mitandaoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents