Burudani

Godzilla akana kuchanganyikiwa kisa kuwa verified twitter

Rapper Godzilla amesema kutumia sana mtandao wa twitter hasa kipindi cha nyuma si ishara ya yeye kuchanganyikiwa kama baadhi ya watu walivyokuwa wakidai.

Godzilla ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma mpya ‘X’, ameiambia Ladha 3600 ya E Fm kuwa account yake kuwa  verified siyo sababu ya kufanya hivyo.

“Kila mtu ana ulevi wake ninapenda kile kitu, lakini siyo kila ninachotweet kinanihusu mimi, naishi na watu na kila mtu ananiambia matatizo yake siwezi yote nikayaweka kwenye nyimbo sometime natweet kwa niaba yao,” amesema na kuongeza.

“Kuwa verified hainitoshi mimi, labda hiyo tiki ya blue inanihukumu lakini siyo chochote, yaani ni alama tu haikupi hata hela. Kwangu ni kama alama kwamba hii account haiwezi kutumiwa na mtu mwingine yeyote kwa biashara, lakini haiwezi kunipa chochote,” amesema Godzilla.

Account ya twitter ya Godzilla ina followers 111k, following 592, tweets 60.7k na likes 13k.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents