Bongo Movie

H Baba, Maunda Zorro watinga Tollywood

Mwanamuziki mkali wa Takeu aliyezimika kiaina, H Baba ameamua kugeukia fani ya uigizaji na kwa mara ya kwanza ataonekana kwenye filamu ya ‘Happy Couples’ akiwa ameshirikiana na nyota wa filamu nchini Yusufu Mlela wakiwemo wengine wengi. Filamu hiyo ya muziki maisha na mapenzi imetayarishwa na kampuni ya Pilipili Entertainment ambayo inasifika kwa kutoa movie za uhakika Bongo. Pilipili Entertainment ni Kampuni iliyo shinda tuzo mbili katika Maonyesho ya Filamu Zanzibar (ZIFF).

 

Happy Couples imewashirikisha waigizaji maafuru nchini Ahmed Ulotu ,Chillo,Techla Malala na hata mwimbaji nyota wa kizazi kipya Maunda Zorro.

Happy Couples ni filamu ya kwanza nchini ambalo jopo zima la watayarishaji wake ni watanzania wenye asili ya kiasia waliobobea katika fani hiyo na kupata hata ujuzi katika fani ya sanaa nchini India.

Sinema hiyo imetayariswa na sameer srivastava pamoja na Sajin Srivastava. Happy Couples imeandikwa na Parves Nageeb ikiongozwa na Ritesh Jadhav na kuhaririwa na Roopendra Raghav.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents