Michezo

Hakuna mchezaji wa Simba atapata namba Yanga – Ali Kamwe

Mtazamo wa Meneja wa Habari ya Mawasiliano wa Yanga SC Ali Kamwe ni kuwa katika kikosi cha Simba SC msimu huu wa 2023/2024 hakuna mchezaji yeyote anayeweza kuingia katika kikosi cha kwanza cha Yanga ya msimu huu.

Kamwe ameyasema hayo alipoulizwa kuhusu mtazamo wake kuhusu Kikosi chao na cha watani wao.

“Were Anglia kuanzia golini, Golikipa wetu mmoja ni sawa na wao wanne labda, hawana uhakika magolikipa wao ndio maana kila siku wanabadilisha, anafungwa huyu kesho wanabadilisha.

“Nenda hivyo hivyo Yao Yao ndiye ana Assist nyingi sasa hivi unaona nani sasa anaweza kuja kuingia kikosi cha kwanza Yanga?? alisema Kamwe.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents