Burudani

Hamisa Mobeto akana kuwa na uhusiano ya kimapenzi na Diamond Platnumz

Mrembo aliyewahi kushiriki miss Tanzania Hamisa Mobeto a.k.a Hamisa kadomo amekanusha tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii kipenzi cha kinadada Naseeb Abdul a.k.a Daimond Platnumz na kusema kuwa anamuheshimu kama shemeji yake.

Hamisa

Hamisa ambaye pia amewahi kuonekana katika video ya msanii Quick Rocka ‘My baby’, ameiambia Global Publishers kuwa maneno yanayosemwa mitaani si ya kweli na wala haitawahi kutokea.
“Kamwe siwezi kutembea na Diamond na haitatokea kwani jamii nzima inajua yupo na Wema na mimi huyo mtu ni rafiki yangu mkubwa, hana chake hapa, siwezi kutembea naye kamwe, namheshimu kama shemeji yangu”.Alisema mrembo huyo.

Mrembo huyo ambaye uzuri wake unazidi kumpa dili kibao ndani na nje ya Tanzania kila kukicha, ameongeza kuwa hana mazoea na staa huyo wa ‘Number One’ na kama kuonana waliwahi kuonana miaka ya nyuma na si kimapenzi.

Source: Global Publishers

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents