Burudani

Hatimaye ndoa ya Kim Kardashian na mumewe wa zamani imetenguliwa rasmi na mahakama, sasa yuko huru kuolewa na Kanye West

Ndoa ya Kim Kardashian na aliyekuwa mumewe mchezaji wa NBA Kris Humphries iliyodumu kwa takriban siku 72 tu imefikia tamati kisheria baada ya talaka kupitishwa.

Kim & humphriez
Humphries na Kim walifunga ndoa mwezi (August 2011), baada ya kukaa kwenye ndoa kwa siku 72 Kim alifungua kesi mahakamani ya kudai talaka kwa sababu za kutofautiana. Kwa kipindi chote hicho toka waachane Humphries ameendelea kuwa single wakati mwenzie Kim Kardashian aliendelea na maisha yake na kuanzisha mahusiano mapya na rapper Kanye West ambao wanategemea kupata mtoto wao wa kwanza soon.

Jumatatu ya wiki hii (June 10) Humphries mwenye miaka 28 alinukuliwa na US Weekly akiwaambia waandishi wa habari kuwa baada ya kuachana ramsi na Kim sasa anaweza kuendelea na maisha yake, hawezi kulazimisha mapenzi, lakini sasa ana furaha na ataendelea kufocus na career yake. “You can’t force a love life, I’m happy. I’ve got a big smile on my face. I’m just focused on training and basketball.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents