HabariMichezo

Hatukwenda Pre-season kujiandaa na Ngao ya Jamii

Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally ametamba kuwa matokeo wanayopata timu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni kutokana na maandilizi mazuri ya ‘Pre-season’ waliyofanya.

Ahmed Ally ameyasema hayo kupitia Wasafi fm wakati huu ambao mashabiki wa soka nchini wameshuhudia Mnyama Simba SC akiondoka na ushindi mnono wa magoli 3-1 ugenini Angola dhidi ya Primeiro de Agosto.

”Tulijiandaa mapema kabisa kushiriki michuano ya Kimataifa, wakati Simba tunakwenda nchini Misri kufanya ‘Preseason’ na kucheza na kina Haras El Hodoud ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya michuano ya kimataifa.”

”Hatukwenda Misri kwaajili ya kujiandaa  na Mtibwa Subar, Ngao ya Jamii, wala kujiandaa na Geita Gold FC, ilikuwa ni kujiandaa kwaajili ya michuano ya kimatiafa.”

”Tukaenda nchini Sudan, tukacheza na Al Hilal, kucheza na Asante Kotoko yote ilikuwa ni kujiandaa na mechi za kimataifa, maandalizi yetu ndiyo ambayo yanatulipa hivi sasa, kwa hiyo ukiachilkia mbali uzoefu tuliyonao lakini vile vile tumefanya maandalizi.”

Simba SC inatarajia kushuka uwanja wa Mkapa siku ya Jumapili katika mchezo wa marudiano dhidi ya waangola hao de Agosto, huku mtani wake Yanga SC akisafiri mpaka nchini Sudan kuwakabili Al Hilal baada ya dakika 90 katika dimba la Mkapa kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Written by @fumo255 (Hamza Fumo)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents