Uncategorized

Henry aomba radhi kwa kumuita beki wa Strasbourg ‘Bibi’ timu yake ikipigwa 5 – 1, ‘Siyo mara yangu ya kwanza kutumia hili neno’

Kocha wa klabu ya Monaco, Thierry Henry ameomba radhi baada ya kumtukana beki wa Strasbourg, Kenny Lala kwa kumuita bibi wakati wa mchezo wao siku ya Jumamosi huku wakipokea kipigo cha mabao 5 – 1 kutoka kwa timu hiyo.

Henry amejutia kosa hilo baada ya kunaswa na camera akimwita mchezaji huyo wa Strasbourg, Lala ‘bibi’ kwenye mchezo wao wa Ligue 1 ambao waliambulia kichapo hicho kibaya cha mabao 5-1.

Tukio hilo lilitokea kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika wakati Strasbourg ikiongoza kwa mabao 2-1 ambapo Lala aliuchelewesha mpira ndipo Henry akanaswa na Luninga ya Ufaransa akitumia lugha ya matusi kwa mchezaji huyo.

“Ndiyo, najutia kwa maneno yangu, ila siyo mara yangu ya kwanza wakati mwingine natumia hata kwa lugha ya Kiingereza,” amesema Henry.

“Nilikuwa nimeghadhibika, samahani sana lakini na mimi ni binadamu.’’

Henry ameanza kibarua cha kuifundisha Monaco mwezi Oktoba huku akifanikiwa kushinda michezo minne pekee kati ya 19 aliyofanikiwa kuiyongoza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents