Michezo

Hongera Yanga kwa mlipofika, tujipange upya

Ni muda mrefu soka la Tanzania kwenye ngazi za vilabu limeonekana kuzorota kufuatia vilabu vyake kutolewa kwenye hatua za mwanzoni za makombe makubwa ya barani Afrika likiwemo kombe la shirikisho na klabu bingwa CAF.

juma-abdul-vs-medeama_q6l271kgyk4z1814t6v3j7cs7

Timu ya Yanga pekee mwaka huu imeweza kupiga japo robo au nusu ya hatua baada ya kufanikiwa kutinga kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho japo wanaonekana kuwa na hali ngumu kwenye kundi lao kutokana na kushika nafasi ya mwisho kwenye kundi hilo huku wakiwa wamebakiwa na mechi mbili pekee ikiwemo ya TP Mazembe ya DR Congo na MO Bejaia ya Algeria.

Hutakiwi kuilaumu timu ya Yanga ilipofika zaidi ya kuwatia moyo wachezaji kwani mwakani wao ndiyo wataendelea tena kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika baada ya kufanikiwa kuibuka mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita.

‘Safari moja huanzisha nyingine’, najua kwa asilimia kubwa wamejifunza mengi mpaka kwenye hatua hii waliyofikia na kutambua wapi walipojikwaa na kuona ni sehemu gani waliyoangukia. Nina matumaini makubwa na timu ya Yanga kufanya vizuri kwa msimu ujao kutokana na wachezaji kupata uzoefu mkubwa na usajili walioufanya kwa kuziba nafasi zenye udhaifu ndani ya timu hiyo.

Mashabiki tulikuwa na matarajio makubwa ya kufanya vizuri kwenye mashindando ya kimataifa kutokana na kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kimataifa akiwemo Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Haruna Niyonzima na Amissi Tambwe huku Juma Abdul, Kelvin Yondani, Deusi Kaseke na wengine ndiyo waliotutia moyo zaidi ya kufanya vizuri lakini bahati haikuwa yetu na uwezo wetu ndiyo ulipofikia.

Kuanza upya siyo ujinga ni bora timu ya Yanga isahau ilipotoka na iangalie wapi iendapo kwa kuanza kwa kujipanga vizuri kwa msimu ujao na hakika itafanya vizuri muda bado upo na uwezo wa kufanya hivyo bado wanao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents