Habari

Polisi aliyekutwa na hatia ya kumuua Mwangosi afungwa jela miaka 15

Askari wa jeshi la polisi kitengo cha FFU, Pacificius Cleophace Simon aliyekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia mwandishi wa Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

MWANGOSII

Hukumu hiyo imetolewa Jumatano hii na Jaji Paul Kihwelo wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa. Mwangosi aliuawa September 2, 2012 kwenye kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi.

Aliuawa wakati wa vurugu kati ya polisi na wafuasi wa Chadema wakati wa maandamano ya kufungua tawi la chama hicho kwenye kijiji hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents