Burudani

Inawezekana American Idol usilione tena, hii ndiyo sababu..

American Idol imekamilika. Kipindi hicho kimekamilika huku mtangazaji wake Ryan Seacrest akikikamilisha kwa mara ya mwisho.

160408111750_american_idol_512x288_bbc_nocredit

Tangu mwaka 2002 kipindi hicho kilisaidia kuzindua ajira kwa wasanii wengi akiwemo Kelly Clarkson na Jennifer Hudson. Ni kipindi kilichopendwa sana katika runinga za Marekani kwa miaka saba mfululizo,huku fainali za kipindi cha mwaka 2003 zikipata watazamaji wengi zaidi ya tuzo za Oscar.

Tamasha la Idol lilianza mwaka 2001 nchini Uingereza,na kumsaidia mfanyabiashara mmoja wa muziki ambaye hakuwa akijulikana Simon Cowel kutawala ulimwengu wa muziki. Wakati huo wazo la kuwasaidia wale wenye vipawa vya kuimba mitaani kuwa nyota halikuwepo.Lakini mafanikio yake nchini Uingereza yalikuwa kiwiliwili kilipoanzishwa nchini Marekani na kuimarika.

Waanzilishi wake walikifanya kipindi hicho kuwa cha msururu wa msimu ,lakini kufikia fainali za msimu wa pili takriban watazamaji milioni 38 walianza kukitazama.

Kwa miaka kadhaa idadi hiyo imepungua ijapokuwa wengi wanasema kuwa kilianguka na kufikia viwango vya kawaida na wala sio vya kupita kiasi.

Hata hivyo mwanzilishi wa tamasha hilo Simon Fuller alisema kuwa Idol huenda ikarudi siku zijazo.

”Bila shaka kutakuwa na mpango mpya uliopigwa msasa wa kipindi hicho.Sasa naweza kukiimarisha na kuleta toleo jipya”, aliongezea.

Source: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents