Habari

Inspekta Haroun amjibu Mh. Temba

Inspekta HarounMWANAMUZIKI mahiri wa kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Halisi la jijini Dar es Salaam, Haroun Kahena ‘Babu’ amekamilisha wimbo mpya unaokwenda kwa jina la ‘Hakuna Mwaka wa Shetani’.

Inspekta Haroun


na Eugenia Kimolo


MWANAMUZIKI mahiri wa kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Halisi la jijini Dar es Salaam, Haroun Kahena ‘Babu’ amekamilisha wimbo mpya unaokwenda kwa jina la ‘Hakuna Mwaka wa Shetani’.


Akizungumza na Tanzania Daima jana, jijini Dar es Salaam, Kahena ambaye pia ni maarufu kwa jina la Inspekta Haroun, alisema kuwa wimbo huo ni maandalizi ya kukamilisha albamu yake binafsi nje ya kundi itakayojulikana kama ‘Natega Mingo’.


Babu alisema kwamba, albamu hiyo itakayokuwa na nyimbo nane, inatarajiwa kuzinduliwa baada ya Sikukuu ya Idd, ambako uzinduzi wake utapambwa na kundi la Wanaume Halisi.


Msanii huyo alizitaja nyimbo zitakazokuwa katika albamu hiyo kuwa ni ‘Binti Kisura’, ‘Za Uso’ aliomshirikisha Issa Shabani ‘Matonya’, ‘Ashura’, ‘Nianzishe’, ‘Haisumbui’, ‘Hakuna Mwaka wa Shetani’ pamoja na ‘Natega Mingo’ aliomshirikisha Juma Kassim ‘Sir Nature’, ambao umebeba albamu.


Babu alisema kuwa, nyimbo za albamu hiyo zimerekodiwa katika studio tatu tofauti, ambazo ni Bongo Records, Up Town Records na Tabasamu Records ya Kenya, ambako amerekodi wimbo ‘Ashura’. Alisema kuwa albamu hiyo ipo bomba na amewataka mashabiki kukaa mkao wa kula ili kupata nyimbo zenye ujumbe kwa jamii.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents