Michezo

Jemedari Saidi afunguka A-Z kuhusu ishu ya Mzize kwenda Azam

Mchambuzi Nguli wa soka Jemedari Said amezungumzia ukweli kuhusu dili la Azam FC na mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize.

“Uongozi wa Azam FC ulipeleka ofa kwa klabu ya Yanga SC wakitaka kumsajili mshambuliaji kinda wa klabu hiyo Clement Mzize ofa ya Azam FC ni Tsh 400,000,000/= (400M), baada ya kupokea ofa hiyo siku iliyofuata Uongozi wa Yanga ukajibu Barua ya Azam FC kwamba wao kama Viongozi watakaa na kujadili Ofa hiyo kisha watawajibu” alisema Jemedari Said.

Kwenye Ofa ya Azam FC hakuna sehemu yoyote ambayo imezungumzia suala la kubadilishana Wachezaji (Swap Deal) kati ya Clement Mzize na Prince Dube ambaye yupo kwenye matatizo na Azam FC.

“Azam FC wamepokea maelekezo ya Kocha wao kwamba anataka washambuliaji 2 mmoja Mzawa na mwengine Mgeni, ndipo Viongozi wa Azam FC wakatoka na Ofa ya 400M, HAKUNA KUBADILISHANA WACHEZAJI” alisema Jemedari Said.

“Kilichotokea baada ya Azam FC kuweka pesa mezani, Mzize kuingiziwa pesa za kuongeza mkataba na klabu yake ya Yanga ambapo bado wapo kwenye Maongezi ya Mkataba mpya”alisema Jemedari.

“Watu wa karibu yake wamethibitisha hili na habari zinasema huenda muda wowote Clement Mzize ataongeza Mkataba na Mabingwa wa Nchi Yanga. Kama ana wasimamizi imara maana yake ni kwamba anaweza kuzoa zaidi ya 400M kutoka Yanga, kwani Azam wako mlangoni. Ila kwa kariba ya wachezaji wetu utakuja kusikia kituko utaziba na Uso” alisema Jemedari Said.

 

NB: Mzize anahusishwa na kutakiwa na Klabu ya Watford ya England, lakini Mzize pia aliwahi kuhusishwa kutakiwa na klabu ya Marseille ya Ufaransa, akili kichwani mwake na wanaomzunguka alisema Jemedari Saidi.

 

 

 

 

 

 

 

 

CC:Tanzaniaweb.Live

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents