Habari

CAG Charles Kichere: Mil 45 za Magufuli Stand hazikuwekwa Bank

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amesema wakati wa ukaguzi wake alibaini kwamba kiasi cha TSh. milioni 45.64 ambazo ni mapato kutoka huduma za hoteli katika kituo cha mabasi Magufuli kwa December 2022 (Sh. milioni 27.32) na Januari 2023 (Sh. milioni 18.32) yaliyokusanywa na Rahabu Logistics Co. Ltd kama Wakala wa ukusanyaji hayakuwekwa katika akaunti za benki za Halmashauri kama ilivyo kwa mujibu wa Agizo la 50 (5) la Memorandamu ya Fedha ya Serikali za Mitaa ya mwaka 2009. Kupitia Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, CAG amesema “Niliomba ripoti za ukusanyaji mapato kwa huduma za hoteli kuanzia February hadi June 2023 lakini hazikutolewa kwa ajili ya ukaguzi na hakukuwa na ushahidi wa kuthibitisha kama mapato yaliyokusanywa wakati huo yalikuwa yameingizwa katika akaunti za Halmashauri”

“Pia, nilibaini kwamba kuanzia February hadi June 2023, Wakala wa ukusanyaji mapato alifanya kazi bila mkataba uliosainiwa na Halmashauri ambao unazua wasiwasi kuhusu masharti na hali za uendeshaji wa hoteli wakati huu, kushindwa kuwasilisha taarifa za ukusanyaji mapato zilizoombwa kwa madhumuni ya ukaguzi, kunapunguza wigo wa ukaguzi kwa ukamilifu wa kutathmini uwazi na usimamizi wa kifedha”

“Ninapendekeza Uongozi uhakikishe TSh. milioni 45.64 zilizokusanywa kutoka katika operesheni za hoteli katika mwezi Decemner 2022 na January 2023 zinatolewa hesabu, pia kuhakikisha kuwa ripoti za ukusanyaji mapato zilizoombwa kuanzia February hadi June 2023, pamoja na taarifa za benki zinawasilishwa kwa wakati kwa ajili ya ukaguzi na kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya Maofisa ambao walizuia kutoa taarifa kuhusu mapato yaliyokusanywa kutoka biashara ya hoteli wakati huu”.

 

 

 

 

 

 

 

 

CC:Millard Ayo.

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents