Michezo

Kesi ya Prince Dube na Azam yaingia Moto

Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji na wanachama ya TFF inakutana kesho Alhamisi Tarehe 18 April 2024 kupitia mashauri tofauti tofauti ikiwemo sakata la mshambuliaji wa Azam FC Prince Dube ambaye amejiweka mbali na klabu hiyo akitaka kuondoka kwa madai mbalimbali yakiwemo ya kimkataba.

Dube aliiandikia TFF barua kulalamika kuhusiana na mkataba wake mpya wa Azam FC kwamba kuna vitu haviko sawa kwahiyo hautambui. Dube ana mkataba na Azam FC ambao unaishia Julai 24,2024 na ndipo unapaswa kuanza mwengine wa miaka 2 mpaka Julai 2026.

Katika kesi hiyo itakayoanza kesho Alhamisi tarehe 18 April 2024 Azam FC watawakilishwa na wakili wa kimataifa kutoka Ureno na ameshawasiliana na TFF kuona uwezekano wa shauri la Prince Dube kufanyika kwa nia ya mtandao (Zoom Meeting) ili aweze kushiriki akiwa huko huko Ureno.

 

 

 

 

 

 

 

 

CC:Tanzaniaweb.Live

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents