Habari

CAG Kichere: DART ikarabati Mabasi 63% ni mabovu

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amesema baada ya uchambuzi wa hali ya uendeshaji wa mabasi ya mwendokasi, amebaini kwamba hadi November 2023, mabasi 132 sawa na 63% hayakuwa yanatumika na yalihitaji ukarabati na matengenezo na kwamba DART ilihusisha NIT katika kufanya ukaguzi na majaribio ya mabasi na kubaini jumla ya TSh. bilioni 2.1 kuhitajika ili kukarabati na kutengeneza mabasi hayo. Kupitia Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka 2022/2023, CAG amesema “Kuwapo kwa idadi kubwa ya mabasi yanayohitaji ukarabati na matengenezo kunavuruga huduma za usafiri wa umma na kusababisha usumbufu kwa abiria na kutopata thamani ya fedha kutokana na kutotumika kikamilifu kwa miundombinu ya BRT” “Kuna huduma ya usafirishaji abiria isiyoridhisha inayotolewa na mtoa huduma wa mpito (UDART), kifungu cha 5 cha Mkataba wa Mtoaji wa Huduma ya Mpito (TSP) – Awamu ya 1 kati ya DART na UDA Rapid Transit (UDART) PLC ambao ulisainiwa tarehe 16 Agosti 2019, kinamtaka UDART kuwa na jumla ya mabasi 140, vilevile, kulingana na Kifungu cha 2.1 cha marekebisho ya 4 ya mkataba ambao ulisainiwa tarehe 5 Agosti 2021, ilikubaliwa kurekebisha mkataba wa TSP kwa kuongeza magari 70 ya mita 18 aina ya “articulated”, na kufanya jumla ya mabasi kuwa 210” “Hii ingemuwezesha mtoa huduma kuhakikisha kuwa 90% ya magari yote yanafanya kazi kwenye njia kuu na ndogo wakati wa nyakati zenye abiria wengi na 10% iliyobaki itatumika kama akiba kwa ajili ya kubadilisha mabasi yanapoharibika” “Ninapendekeza kwa Menejimenti ya DART kuchukua hatua za haraka kupata fedha ili kufanikisha ukarabati na matengenezo ya mabasi, na kuhakikisha upatikanaji wa vipuri vya kubadilisha na kuwa na ratiba ya matengenezo ya mara kwa mara”.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

CC: Millard ayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents