Habari

Jeshi la polisi kuanzisha msako kwa wanaomiliki silaha kinyemela

Jeshi la polisi limepanga kuanza msako wa kutafuta silaha zinazomilikiwa na raia kinyume na taratibu kuanzia Novemba 22 mwaka huu hadi Disemba 20 mwaka huu baada ya wananchi wanaomiliki silaha kushindwa kujitokeza kwenye zoezi la hiari la uhakiki wa silaha zao.

1

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa hii, jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa makosa ya jinai, Kamishna Robert Boaz, amesema mpaka sasa silaha zilizoletwa kuhakikiwa ni asilimia 59.18 wakati silaha ambazo bado hazijahakikiwa sasa ni zaidi ya asilimia 40

“Tunatambua zipo sababu mbalimbali,ukubwa wa nchi, kupata taarifa, pengine mwananchi alikuwa nje ya nchi, sasa tunatoa grace period (muda wa rehema mwingine)ambao hautaongezwa baada ya hapo kuanzia tarehe 22 ya mwezi huu hadi tarehe 20 ya mwezi wa 12 mwaka huu tutaendelea kupokea silaha kwaajili ya uhakiki na baada ya hapo hatutaongeza muda mwingine tena,”alisema Boaz.

Aidha kamishna Boaz amezungumzia adhabu kwa wale wote ambao hawajajitokeza kupeleka silaha zao ili kuweza kuhakikiwa huku akisema hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.

“Baada ya hapo yeyote ambaye ana silaha anaimiliki kwasababu moja au nyingine hajataka kujitokeza, tutafuta leseni ya silaha zote ambazo hazijahakikiwa. Na baada ya hapo tutatangaza majina ya watu wote ambao hawajahakiki silaha zao kwasababu rekodi tunazo na mwisho tutafanya msako nyumba kwa nyumba na kwasababu tunawafahamu ni nani ambao wanamiliki silaha, tutawachukulia hatua za kisheria,” alionya.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents