Habari

Jokate azindua ‘Jokate Club’ ili kuwa karibu na jamii katika mitindo

Mwanamitindo, mbunifu na Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, Jokate Mwegelo ameanzisha klabu yake ijulikanayo kwa jina la ‘Kidoti Club’.

Jokate akiwa na Boke.
Jokate akiwa na Bhoke.

Akizungumza katika uzinduzi wa klabu hiyo leo uliofanyika Mikocheni jiji Dar es Salaam, Jokate alisema Kidoti Club ni tofauti na vilabu vingine kwani katika ujio wake huo mpya, atakuwa akijihusisha na mambo mbalimbali katika jamii hususani masuala ya urembo na mitindo.

Jokate akisomea ujumbe uliopatikana baada ya mwanadada huyo kupokea ujumbe baada ya kujiunga na Club ya Jokate.
Esther Wassira (kulia) akisoma ujumbe mara baada ya kujiunga na Club ya Jokate, katikati ni Jokate na wa kwanza kushoto ni Bhoke wa EATV

“Huu ni mfumo wa kisasa katika kutoa taarifa mbalimbali kwa jamii. Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu anayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu yake. Mimi pia naelekea huko kwani nitaweka taarifa zangu mbalimbali na ili kupata lazima uwe mwanachama,” alisema Jokate ambaye pia ni mtangazaji na mbunifu wa mavazi.

“Kama unavyojua, lengo langu kubwa ni kutumia ujuzi na kipaji changu kwa watanzania wote, nataka wafaidike na vipaji vyangu nami kusimama mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu yoyote. Natoa wito kwa vijana wenzangu kuwa wabunifu katika kukabiliana na masuala mbalimbali ya maisha.”

Jokate akifanywa maker up ndani ya Milionea Soloon Mikocheni jijini Dar  baada ya kuzindua Club.
Jokate akifanyIwa make- up ndani ya Milionea Soloon Mikocheni jijini Dar baada ya kuzindua Club

Alisema lengo lake kubwa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na anaamini watu wengi watajiunga naye. Ili uwe mwanachama wa klabu hiyo, unatakiwa kutuma neno kidoti kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.

Jokate alisema kuwa kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri mbal mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwaajili ya rika tofauti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents