Burudani

Kamati ya Miss Tz yadaiwa kushindwa kukamilisha mahitaji ya Happiness kwenda Miss World

Mama mzazi wa Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa ameitupia lawama kamati ya Miss Tanzania kwa kushindwa kutimiza mahitaji ya mtoto wake ili kumwezesha kwenda kushiriki mashindano ya Miss World.

Mshindi wa Miss Tanzania 2013 Happyness Watimanywa akiwa na Mama ake Mzazi
Mshindi wa Miss Tanzania 2013 Happyness Watimanywa akiwa na Mama yake mzazi

Akizungumza na E-newz wa Eatv leo, Mama Happiness amesema amekuwa akifatilia kwa kamati hiyo lakini wamekuwa wakimzungusha.

“Wanasema hiki wanasema hiki, kwamfano kama introduction shooting wakasema kwamba is very expensive,kwahiyo mimi nikajitolea nikalipa milioni moja down payment, tangu mwezi wa tano nilikuwa nawaambia mpaka two weeks ago hawana jibu lolote, mimi naogopa mwanangu asije akashushwa kwenye stage, wewe huna visa hauruhusiwi kuja kushiriki shindano hili. Haya hela ya shooping ambayo ni shilingi milioni tano walipaswa wamlipe mtoto mpaka leo bado siku mbili mtoto anaondoka Jumamosi leo wanamkabidhi tiketi bado hawajampa hela ya shooping sasa mtoto anaendaje bila maandalizi, ndiyo maana nchi yetu kila mwaka inakuwa ya mwisho,” alisema Mama Happiness

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents