Burudani

Keisha atangaza nia rasmi, aomba mashabiki wamsaidie kwenye safari yake katika siasa

Muimbaji wa ‘Usinitenge’ Keisha naye ameungana na wasanii waliotangaza nia ya kuwania nafasi za uongozi mwaka huu.

keisha

Keisha amesema ana nia ya dhati ya kugombea ubunge na anahitaji msaada wa hali na mali kutoka kwa mashabiki wake.

“Najua wengi mnajiuliza maswali mengi sana juu yangu kwanini nimeamua kuingia kwenye siasa lakini leo naomba nifunguke na kuwaambia kitu,” ameandika kwenye Instagram.

“Mimi kama mlemavu wa ngozi najikubali najipenda na ninajiamini lakini yote tisa napigana kwa uhuru na amani ambayo tunastahili kuipata kutoka nchini kwetu.nilipoanza kupost picha zangu za siasa kuna ambao walinipongeza na kuna ambao walinisema kwamba sina uchungu na wenzangu kwakuwa wanahisi nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe mimi ni mpiganaji na ndomana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu. Fimbo ya mbali haiui nyoka na kidole kimoja hakivunji chawa nikimaanisha kwamba lazima tusimamie sheria ambazo zitatusaidia kuendeleza amani hivyo basi lazima tuwe na wawakilishi wa kutosha ndani ya bunge ili sauti zetu zisikike ili sheria kutungwa na kutekelezwa pia,” ameongeza.

“Hivyo mimi kama mtanzania mwenzenu nahitaji support yenu ili niweze kufikia malengo yetu kwa yeyote ambaye anaupendo nasi na mimi na harakati zangu anisaidie kwa chochote ambacho kitanifikisha nnapoataka this is my tigo no 0718785045 na hii ni account number yangu ya crdb 011 2022295800 jina ni Hadija Shabani Taya unaweza kuchangia humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents