Burudani

Kinachomtatiza Madee katika Bongo Flava

Msanii wa muziki Bongo, Madee amesema wasanii wana nafasi kubwa ya kutangaza biashara mbalimbali lakini kitu hicho hakipewi sana nafasi katika Bongo Flava.

Madee amesema duniani kote wasanii wamekuwa wakitangaza kampuni za kibiashara kitu ambacho Bongo kinachukuliwa kawaida na kupewa nafasi ndogo.

“Wasanii wana nafasi kubwa sana ya kutangaza makampuni lakini sijajua kwanini hapa nyumbani inakuwa ngumu sana, kwa upande wa wasanii inakuwa haipo hiyo,” Madee ameiambia Radio One.

“Japo tunaona mara chache chache inaweza ikatokea kampuni ikadeal na msanii fulani then baada ya mwaka mmoja/miwili hatumsikii tena lakini naamini unapofanya biashara unataka faida sasa labda hiyo kampuni ilikosa kile ambacho walidhani watakipata,” ameongeza.

Madee kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Sema’ ambao amemshirikisha Nandy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents