Habari

Kitendo cha mke kumnyima unyumba mume chazua mjadala mzito Malaysia

Mbunge mmoja nchini Malaysia amekosolewa vikali baada ya kusema kuwa wanawake wanaowanyima mabwana zao tendo la ndoa huwasababishia dhuluma za kisaikolojia.

Che Mohamad Zulkifly Jusoh kutoka chama tawala cha Barisan Nasional, alikuwa akizungumza wakati wa mjadala wa bunge kuhusu dhuluma za nyumbani.

Malaysia iko katika mikakati ya kufanyia sheria marekebisho kutatua dhuluma za nyumbani.
Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 58 kutoka jimbo la Terengganu, alisema kuwa wanaume wanapitia kwa asilimia kubwa dhuluma za kisaikolojia kuliko zile za kimwili.

“Licha ya wanaume kuwa wenye nguvu kuliko wanawake, wanawake huwadhulumu katika masuala kama haya kwa njia iliyo ya kuumiza,” alisema Jusoh.

Wanasiasa na makundi ya wanaharakati yana matumaini kuwa mswaada mpya utawakinga zaidi waadhiriwa wa dhuluma za nyumbani.

Pia ni halali nchini Malaysia, nchi yenye waisilamu wengi kwa wanaume kuoa hadi wake wanne ikiwa watapata idhini kutoka kwa mahakama za sharia.

Bwana Che aliliambia bunge kuwa kumyima mwanamume muislamu haki ya kuao mke wa pili ni sawa na kumdhulumu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents