Burudani

Lil Wayne na Birdman sasa mambo fresh

Huenda beef kati ya Lil Wayne na Birdman limemalizika mara baada ya wawili hao hivi karibuni kuonekana wakiwa pamoja katika matukio mbali mbali.

Utakumbuka March 11 mwaka huu wawili hao walionekana wakisalimiana walipokutana katika Night Club mjini Miami.

Leo March 26 Birdman ameposti picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa na Lil Wayne na kuandika; Me and my SON #YMCMBEAST.

Video: Lil Wayne na Birdman walivyokutana Club

Hapo awali wawili hao walikuwa katika beef zito, chanzo cha beef lao ni kuhusu album ya Lil Wayne  ‘Tha carter V’ ambayo haikutoka kitu kilichopelekea Lil Wayne kufungua kesi dhidi ya Cash Money Records mwaka 2015.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents