Michezo

Marcus Rashford kuziba nafasi ya Rooney na Kane timu ya taifa Uingereza

Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Marcus Rashford anatarajiwa kuwa kwenye kikosi cha kocha wa Uingereza, Gareth Southgate.

Kiungo huyo ambaye ana umri wa miaka 19 hapo awali alitarajiwa kushirikishwa katika upande wa vijana mwenye umri chini ya miaka 21 watapokuwa wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani na Denmark wikendi ijayo.

Lakini washambuliaji wa England Harry Kane na Wayne Rooney wote wametolewa kutokana na majeraha , huku Rashford akitarajiwa kuchukua nafasi hiyo.

England itapamba na Ujerumani katika mechi ya kirafiki kabla ya mchuano wa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania huko Wembley tarehe 26 mwezi Machi.

Rashford ambaye mechi yake ya kwanza kuichezea Uingereza alifunga goli walipopata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Australia mwezi Mei mwaka Jana na wamejizolea vikombe sita vikuu.

Manchester United ilimchezesha waliposhindwa kwa bao 1-0 dhidi ya Chelsea katika kombe la FA siku ya Jumatatu , licha ya kutolewa katika kikosi cha hapo awali kutokana na maradhi.

Nahodha wa Uingereza, Rooney alikuwa nje wakati Manchester United ilipo kutana na Chelsea kutokana na jeraha alilolipata alipogongana na mwenzake walipokuwa wakifanya mazoezi.

Na mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane pia alitolewa nje ya uwanja kutokana na jeraha la kifundo cha mguu walipokuwa wakicheza na Millwall siku ya Jumapili.

Klabu ya Spurs imesema jeraha hilo linafanana na lile alilolipata mwezi Septemba wakikabiliana na Sunderland.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents