Mitindo

Maznat atoa somo kupitia Wema Sepetu na Aunt Ezekiel (+video)

Mjasiriamali Maznat Bridal ametoa somo kwa kina dada ambao wanatamani kufikia mafanikio kwa njia ya mkato kwa kueleza kuwa mchakato wowote wa mafanikio lazima unachukua muda.

Maznat ambaye pia ni motivation speaker amesema hayo hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa nguo mpya za Mwanamitindo Khadija Mwanamboka.

“Kuwa makini katika kutumia muda wako, mtu yeyote anayekupotezea muda wako achacha naye, fanye kazi kwa bidii lakini pia ujifunze kuweka akiba ya hela. Watu wengi wanafanya biashara ndogo ndogo wakishazipate zile hela wanatumia hapo hapo” amesema Maznat.

“Anataka kufanana na dada Wema, Aunt Ezekiel, no!! mpaka anafikia hapo alipo amechukua muda kufika. Pia wawe na mipango sahihi, kabla mwaka hujanza apange mipango yake, atumie muda wake vizuri na lazima utatoka” amesisitiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents