Habari

Mfanyabiashara alipa Tsh Mil 24 Halmashauri wao wameandika Mil 3 (Video)

“Mimi napigika usiku na mchana nafanya kazi, najaribu kusaidia nchi yangu nalipa kodi wao hawana hata taarifa kama nimelipa”

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Paul Christian Makonda @baba_keagan Jumamosi hii amefanya Kikao na Wadau mbalimbali wa Utalii Mkoani Arusha na kuagiza kuundwa kwa Kamati maalum ya kufuatilia na kutafuta Muarobaini wa Changamoto zinazoikabili sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Arusha.

Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkoa,kimewakutanisha Maafisa mbalimbali wa idara za utalii na sekta mtambuka zinazohusiana na Utalii huku Wadau wakipata fursa ya kueleza changamoto walizonazo mbele ya Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda.

Miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa ni pamoja na usumbufu na mifumo isiyoeleweka ya ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali za serikali pamoja na matumizi makubwa ya nguvu kwenye kudai kodi na tozo za serikali.

Aidha changamoto ya mifumo inayotumika na Mamlaka ya Mapato kwenye kudai Kodi ni miongoni mwa Mambo yaliyozungumzwa na kudaiwa kusababisha uombaji na utoaji wa Rushwa.

Aidha Mkuu wa Mkoa pia amewataka maafisa wa serikali wanaoshughulika na utalii ikiwemo Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na ile ya Wanyamapori kuandaa matamasha mbalimbali ili kukuza uelewa wa vivutio vinavyopatikana Mkoani hapa.

Katika hatua nyingine pia Mh Makonda amesisitiza kuhusu uimarishaji usalama ndani ya Jiji la Arusha ili kuvutia zaidi watalii na wageni mbalimbali kuweza kutembelea mkoa wa Arusha bila ya kuhofia chochote.


Mkuu wa mkoa pia amesisitiza suala la usafi katika Jiji la Arusha na kumtaka kila mwananchi wa Arusha kuwajibika kuyaweka mazingira yake katika usafi.

Mkuu wa Mkoa pia ametoa wito wa kuzipenda na kuzithamini familia akisema kwamba utulivu na mapenzi ndani ya familia huchagiza Ufanisi na ustawi tuwapo katika kazi zetu za kila siku ama katika shughuli za uzalishaji mali.

Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda amekutana na wadau hao wa Utalii ikiwa ni Mwanzo wa kufahamiana na kujenga Msingi mzuri katika kutekeleza agizo la Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan la kumtaka kukuza Utalii jijini Arusha.

Written by @yasiningitu

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents